MADA YA SITA: ANDISHI WA INSHA NA MATANGAZO
MADA YA SITA: ANDISHI WA INSHA NA MATANGAZO Uandishi wa Insha za Kisanaa Misingi ya Kuandika Insha Insha za kisanaa ni insha zinazoelezea mambo ya kawaida katika jamii lakini kwa kutumia lugha ya kisanaa. Lugha ya kisanaa ni pamoja na matumizi ya tamathali za semi, misemo nahau, methali na taswira. Muundo wa Insha Kwa kawaida insha inakuwa na sehemu kuu nne: kichwa cha insha, utangulizi, kiini na hitimisho. Kichwa cha insha; Kichwa cha insha hudokeza kile utachokijadili katika insha yako, hubainisha wazo kuu la mada inayohusika. Kwa kawaida kichwa cha insha huandikwa kwa sentensi fupi. Mfano; maisha ya kijijini, mimba za utotoni. Utangulizi; Mambo yaliyopo katika utangulizi ni pamoja na kutoa fasili ya maneno muhimu na kuelezea kwa muhtasari mambo ambayo utakwenda kuyajadili katika insha yako. Utangulizi unakuwa katika aya moja fupi. Kiini cha insha; Katika kiini ndipo kuna maelezo ya kina juu ya kile unachokijadili katika insha yako, maelezo haya yanakuwa...